SectionsExitZungukazunguka

Zungukazunguka

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Mbinguni kwa Baba, kweli kuna raha,

Makerubi wote hata maserafi

Malaika wote na watakatifu,

Wako mbele za Mungu kila mtu na kazi yake

Chorus

Waimbaji tutaimbaimba, tutaimba nyimbo za shangwe

Malaika watarukaruka, wataruka mbele za Mungu

Watu wote (kweli) watafurahi nyumbani mwa Bwana

Watacheza (wote) pamoja wakizungukazunguka

Verse 3

Tuimbe nyimbo nzuri kama makerubi,

Tuimbe kwa furaha kama maserafi

Na tuchezecheze kama watakatifu,

Tukirukaruka kama malaika wa Mungu

Verse 4

Wenye moyo safi na matendo mema,

Twendeni kwa Baba tupate dhawabu

Tumekaribishwa Mbinguni kwa Baba

Twendeni tuone, jinsi tulivyoandaliwa.

Verse 5

Sisi tunaimba nyimbo za Mbinguni,

Tena twatabiri yale ya Mbinguni

Yote yalopita kwa wenye hekima,

Tumefunuliwa, tutangaze kwa nyimbo hizin

Verse 6

Fanya utafiti na upeleleze,

Utafunuliwa siri za Mbinguni

Waloshinda vita, wateule wa Mungu

Wanatungojea kwenye raha ya siku zote