Zawadi Tosha

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Chorus

Nimetunukiwa tuzo lenye thamani

Nimeletewa zawadi toka mbinguni

Nimejishindia Mwana wa Mungu

Nimepewa Yesu zawadi tosha

Verse 2

Ninashangilia naimba kwa furaha

Ninarukaruka nacheza kwa furaha

Napiga makofi na vigelegele

Nimempata Yesu tuzo la ajabu (mimi)

Verse 3

Ninakushukuru ee Mungu Baba yetu

Nasema asante kwa mema yako yote

Napiga filimbi, ngoma na kayamba

Nimejishindia Bwana wa mabwana

Verse 4

Nikiwa na Yesu, magonjwa yamepona

Nikiwa na Yesu mashaka yamekwisha

Yesu kiongozi, Yesu Jemedari

Yesu mchungaji, Yesu mambo yote

Verse 5

Maisha marefu ni tuzo nimetuzwa

Uzima milele nimeshaahidiwa

Mbinguni kwa Baba nitakaribishwa

Nitaishi vyema siku zangu zote