SectionsExitZanena Siku Kuu

Zanena Siku Kuu

ChristmasExit
Verse 1

Zanena, siku kuu,

Kengele za juu,

Waumini furahini,

Mkombozi mkumbusheni

Mzawa leo Bethlehemu

Mzawa leo Bethlehemu

Verse 2

Ni hii leo, siku heri,

Siku nzuri nzuri,

Ya uasi kuondolewa,

Ya mbingu kufunguliwa

Yakisha maulaumu,

Yakisha malaumu

Verse 3

Ni hii leo, siku njema,

Siku ya salama,

Aliposhuka Mwokozi,

Mwanaye Mungu Mwenyezi

Kuwa mwanadamu,

Kuwa mwanadamun

Verse 4

Leo siku, hakika,

Wala hamna shaka

Kwamba dhambi ya asili,

Yaweza kufutwa kweli

Ina dawa timamu,

Ina dawa timamun

Verse 5

Leo siku ya neema,

Yameshuka mema

Asifiwe Mungu juu,

Watu wa imani kuu

Waletewa amani,

Waletewa amani