Ee Mungu ukifuatilie kilio chetu
Nazo sala kwa ajili ya usalama wetun
Ni wewe uliye tegemeo utulinde daima milele
Kwako tumejikabidhi, utulinde daima milele
Ulivyowavusha Wayahudi, utulinde daima milele
Baharini kwa miguu, utulinde daima milele
Ukumbuke ahadi yako, utulinde daima milele
Aombaye utampa, utulinde daima milele
Tumekuita na kwa sauti na kwa machozi mengi
Uko kimya lakini twajua utaitika
Wanaotupenda wameungana kutuombea
Usiache magoti yao yachubuke bure
Malaika na watakatifu wanatuombea
Wasikie kwa sababu umependezwa nao
Yakumbuke maumivu ya Yesu msalabani
Ukubali yawe badala ya mateso yetun
Tunakwama sauti makoo yamechoka
Fanya hima mwenyezi uje utuokoe
Hayatoki machozi ona yamekauka
Tutalia na nini wahi utuokoe
Ewe Rabi Mungu yowe la Mwisho tunapiga utusikie * 2
Ewe Rabi Mungu yowe la Mwisho tunapiga uwiii
Yowe la Mwisho tunapiga utusikie