Chorus
n{ Yote yaliyokupata ni mapenzi ya Mungu
Usilalamike wala usivunjike moyo } * 2
Verse 2
Ayubu aliteseka alivumilia
Hakulalamika wala hakuvunjika moyo
Verse 3
Shida iliyokupata yote itakwisha
Usilalamike wala usivunjike moyon
Verse 4
Magonjwa uliyo nayo yote yatakwisha
Usilalamike wala usivunjike moyo
Verse 5
Umepatwa na msiba ni mapenzi ya Mungu
Usilalamike wala usivunjike moyo
Verse 6
Kazini umefukuzwa zidisha maombi
Usilalamike wala usivunjike moyon
Verse 7
Ushukuruni kila jambo linalokupata
Baba yetu wa Mbinguni akungoja pema