SectionsExitYesu Yupo

Yesu Yupo

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Yakija mawimbi hata dhoruba ikizidi

Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu

Upepo mkali hata bahari ichafuke

Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu

Verse 2

Ni yeye Yesu alitembea juu ya maji (sikia)

Akamuita Petro ashuke akamfuate

Na hata Petro alipojawa na wasiwasi (sikia)

Yesu akawa pamoja naye na kutulia

Verse 3

Nami ninayaacha niyasafiri nayo (sikia)

Nashuka nikamfuate Yesu niende naye

Nijapopatwa na misukosuko katikati (sikia)

Sitateteleka kwani Yesu yu pamoja nami

Verse 4

Nitayatimiza yote atakoyonipa

Yesu ni wangu nami ni wa Yesu najivunia