SectionsExitYesu Wa Vituko

Yesu Wa Vituko

MarianExit
Verse 1

Huyu ndiye Yesu wa miujiza nauliza

Huyu ndiye Yesu wa maajabu nauliza

Aliyegeuza maji kuwa divai

Kwenye harusi kule Kana Galilaya

Chorus

Huyu ndiye Yesu, (Yesu) Mwana Wa Mungu

Huyu ndiye Yesu, (Yesu) kutoka Mbinguni

Huyu ndiye Yesu, aliyekuja kwetu

Huyu ndiye Yesu mwenye upendo mwingi

Verse 3

Huyu ndiye Yesu Mnazareti nauliza

Huyu ndiye Mwana wa seremala nauliza

Aliyewaita wavuvi wa samaki

Akawageuza wavuvi wa watun

Verse 4

Huyu ndiye Yesu mwenye huruma nauliza

Huyu ndiye Yesu Simba wa Yuda nauliza

Aliyewakemea mapepo kwa nguvu

Aliyewaamuru mapepo watoken

Verse 5

Huyu ndiye Yesu mwenye baraka nauliza

Huyu ndiye Yesu mwenye chakula nauliza

Aliyewalisha watu elfu tano

Kwa mikate mitano na samaki wawili

Verse 6

Huyu ndiye Yesu mwenye vituko nauliza

Huyu ndiye Yesu asiyeshindwa nauliza

Aliyewatimua watu hekaluni

Walipogeuza hekalu kuwa soko

Verse 7

Huyu ndiye Yesu mwenye hekima nauliza

Huyu ndiye Yesu mwenye elimu nauliza

Aliyeng'amua hila zake shetani

Pale nyikani alipojaribiwa