Verse 1
Yesu mwema najitolea kwako
Kwa leo hii na siku zote
Nafsi yangu na moyo wangu wote
Heri kweli, heri kweli
Heri kweli raha ya uwingu x2
Ndani mwangu umekuja daima
Kuwa nami ni upendo wako
Verse 2
Ewe mpenzi mwenye utamu mwingi
Ni mapendo, ni mapendo
Ni mapendo ya moyo wako x2
Verse 3
Nitaweza kukurudishia nini
Kwa wema huu na pendo lako
Roho yangu umeifadhilia
Nikupende, nikupende
Nikupende ni tama yangu x2
Verse 4
Weka Rabi katika roho yangu
Wema wako na unyenyekevu
Na pendo kuu fadhila na amani
Niongoze, niongoze
Niongoze katika amani x2