SectionsExitYesu Kristu Atawala

Yesu Kristu Atawala

MarianExit
Chorus

Yesu Kristu atawala milele yote

Yesu Kristu ndiye Bwana wa mabwana wote

Yesu Kristu atawala milele yote

Yesu Kristu ni mfalme wa wafalme wote

Chorus

Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliyetukomboa kwa damu yake

Mataifa njooni tumwimbie

Tumfanyie shangwe Mungu wetu

Tuzitangaze rehema zake, pia na utukufu wake

Ili mataifa yote duniani

Yapate kumjua Bwana

Nao wote waliopotea, waweze kumrudia Mungu

Verse 3

Alikuja duniani, kwa ajili yao,nili mi niliye mdhambi nipate kuokolewa

Alipata mateso mengi kwa ajili yangu mimi

Verse 4

Tazama uwezo wake, Mwana wa Mungu

Limfufua Lazaro kutoka katikati ya wafu

Tazama na yule kipofu, alimponya akapona

Verse 5

Alifanya miujiza mingi duniani

Alitoa pepo wachafu, aliponya na wagonjwa

Aliyakemea mawimbi, bahari ikawa shwarin

Verse 6

Njoo sasa ndugu yangu, kwake Bwana Yesu

Tatizo lako lolote ulilo nalo litakwisha

Njoo ufanyiwe maombi kwa Yesu yote yawezekana