SectionsExitYesu Ateswa Msalabani

Yesu Ateswa Msalabani

LentExit
Verse 1

Tunapoona Bwana Yesu kuteswa msalabani

Tunasikitika kweli

Kwani tumekusulubu ee Bwana utuhurumie

Verse 2

Dhambi zetu nyingi sana asili ya mateso

Watupenda mpaka mwisho

Umekufa tuokoke ee Bwana utuhurumie

Verse 3

Tunapona msalabani sawa na mwizi mbaya

Ulitaka kutukanya

Tuyaache majivuno, ee Bwana utuhurumie

Verse 4

Tunapoona msalabani miiba yachoma kichwa

Unalipa kwa matesa

Fungua na tamaa zetu ee Bwana utuhurumie

Verse 5

Msalabani, umefungwa na mikono ya damu

Mkono wako wenye heri

Utujaze na baraka, ee Bwana utuhurumie

Verse 6

Mwili wote wafunikwa, na damu ivujayo

Damu yako isafishe

Uovu wote wa rohoni, ee Bwana utuhurumie

Verse 7

Moyo wako umetonwa, mlango sasa wazi

Tutakase tuingie,

Tukae moyoni mwako, ee Bwana utuhurumie