Verse 1
Yesu alia msalabani. Asikitika juu ya dhambi zetu
Asulubiowa asiyekosa kwamba yeye ni mosaji
Chorus
Ee mwanadamu lipi ambalo linalonipasa kuwatendea
Ambalo sikuwatendeeni, hata ikanipasa msalaba
Verse 3
Magonjwa yote aliyaponya, wafu nao aliwafufua
Kundi la watu aliwaponya, lipi alilokosa
Verse 4
Watu wa Mungu Bwana alia asikitika juu ya dhambi zenu
Asulubiwa asiyekosa kwamba ni mkosaji
Verse 5
Wana wa Mungu, Bwana alia, asema nyinyi mwamsulubisha,
Msipobeba misalaba yenu kwani nyinyi m wakosaji
Verse 6
Tazama Bwana akulilia, akuita ndipo akuokoe
Tazama haya mapenzi yake Bwana hayana mwisho