Verse 1
Tulieni ndugu zangu niwaambie siri moja
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote
Japo magumu ni mengi mtakayokutana nayo
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote
Chorus
{ Mtavuka vikwazo vya shetani na magumu yote (nasema)
Mbinu zake shetani na hila hazitawaangusha (nasema)
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote } *2
Verse 3
Kwa nguvu za Mwenyezi nasema hamtaaibika-
Mtautimiza huu wito wenu kikamilifu -
Verse 4
Mungu Baba yuko nyuma yenu anawapigania-
Atawafukuza na maadui wenye hila mbaya .
Verse 5
Wosia ninawapa ndugu muwe na uvumilivu-
Kwani haya ya dunia si kitu wala si lolote .