SectionsExitWimbo Mkuu

Wimbo Mkuu

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Kwa zaburi, kwa zaburi, kwa furaha, kwa furaha

Tunaimba, tunaimba wimbo mtamu, wimbo mzuri

Kwa sababu wastahili kushangiliwa ewe Mfalme pokea wimbo mkuu

Verse 2

Kwa vinanda, kwa vinanda, na vinubi, na vinubi

Tunaimba, tunaimba tenzi tamu, tenzi safi

Kwa sababu wastahili kushangiliwa ewe Mfalme pokea wimbo mkuu

Verse 3

Mababu zetu waliimba, na wakaturithisha kuimba

Kuimba (kuimba), kusifu (masifu), kusifu asubuhi na jioni sifa

Masifu, sifa, sifa, sifa heshima nao utukufu kwako wewe

Verse 4

Tunakuimbia wimbo mkuu tukiwa chini tunaimba

Ulimwenguni tunaimba, udhaifuni tunaimba

Mbinguni juu malaika nao wanaimba wimbo mkuu

Wimbo mkuu waimba aaa aaa aaaaaaaaaaaanaah aaa wanaimba ooo ooo ooo malaika wanaimba

Mbinguni na watakatifu wanaimba,

Ni raha sana kuimba wimbo mkuu

Ni juu kwa wabarikiwa nao wasafi sana waimba wimbo mkuu

Verse 5

Tujaze nguvu tukuimbie, utuongoze tusiregee

Yote yakatishayo tamaa yafukuze mbali yaondoke

Tamaa yetu tukuimbie na binadamu ulimwenguni

Mwisho tuimbe na malaika milele Mbinguni wimbo mkuu

Verse 6

Watu wote duniani wasikie

Malaika wote wasikie

Na watakatifu wote wasikie

Na wakuimbie kwa sauti tamu

Wanyama na ndege wote wasikie

Bahari na vyote pia wasikie

Nyakati zote wote wasikie

Twakuimbia wimbo mkuun