Waumini Simameni
Ordinary Time,MarianBible Procession
Verse 1
Waumini simameni - tupeleke neno lake
Neno lake Bwana Mungu - ni nuru ya ulimwengu *2
Chorus
Tulisome kweli (kweli kweli)
Tulihubiri sana(biri sana)
Tulisambaze kote na tulifundishe kweli
Chorus
Tulisome kweli (kweli kweli)
Tulihubiri sana(biri sana)
Tulisambaze kote na tulifundishe
Verse 4
Ni neno la Bibilia - kutoka kwa Mungu Baba
Anena kwa kinywa chake - na kwa maandiko yake *2n
Verse 5
Ni dawa ya mioyo yetu - tulizo kwa watu wote
Tulipokeeni leo - tupate kunusurika *2n
Verse 6
Tuchezeni kwa furaha - nderemo na kwa vifijo
Kwa ngoma na tarumbeta - kayamba hata vinanda
Verse 7
Milima iyumbeyumbe - miti na ichezecheze
Bahari ivume sana - mito ipige makofi *2