Verse 1
Watumishi wake Baba wangapi waliopo
Wanakula na kusaza chakula chake Baba.
Chorus
Nami - Nami nataabika hapa,
Nashi - Nashiriki na nguruwe,
Chaku - Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi
Nita - Nitarudi na kusema,
Baba - Baba yangu nisamehe,
Nime - Nimekosa kwake Mungu,nna mbele yako, Baba.
Verse 3
Baba kamuona yu mbali,nkashikwa na huruma:
Akakimbia kumlaki, kamkumbata na busu
Verse 4
Baba sistahili tena kuitwa mwana wako;
Unifanye kama mmoja wa watumishi wako.
Verse 5
Baba yangu, nimekosa, ninaomba huruma;nunisamehe, nirudi, nikakutumikie.
Verse 6
Nasogea ninakuja, ninakukimbilia,
Mimi ni mtoto mpotevu, Baba unipokee.
Verse 7
Wanikaribisha mimi kwenye karamu yako,nmeza imeandaliwa, inaningoja mimi.