Verse 1
{Watu hawatalingana (daima), watatofautianan(nayo ni) makusudi yake Mungu, jina lake litukuzwe } *3
Chorus
{ Sote tumeumbika tulivyo (kadiri) ya mapenzi yake Mungu
Ili utukufu wake Mungu (Mwenyezi) ujulikane kwa wote } *2
Verse 3
Kweli wanadamu wote (hakika) tumeumbwa kwa udongon(hivyo) asili yetu ni moja, tumetoka mavumbini
Verse 4
Wapo walio wanyonge (lakini), pia wapo wenye nguvun(kusudi) Mungu kawaumba hivyo, ili wahudumiane
Verse 5
Wengine kawabariki (sana), amewajalia malin(lakini) wengine amewashusha, wamekuwa hohe hahe.
Verse 6
Wale walio tajiri (kamwe), wasiwanyime fukaran(kwani) maskini wahitaji, huruma ya matajiri
Verse 7
Wote tu wana wa Mungu (hivyo) tuonyeshane upendon(ili) Mungu wetu atukuzwe, sasa na hata milele.