Chorus
Watoto wa Mayahudi walimlaki Bwana
Wakiyachukua matawi ya mizeituni
Wakipiga kelele wakiseman(Hosanna *2 juu Mbinguni )*2
Verse 2
Dunia ni ya Bwana na vitu vyote vilivyomo
Dunia nzima na watu wote waliomo
Kwa maana yeye ameisimika juu ya bahari
Akaithibitisha juu ya mito
Verse 3
Inueni vichwa vyenu, enyi malango
Inukeni, enyi malango ya kale
Mfalme wa utukufu apate kuingia
Ni nani mfalme wa utukufu?
Bwana mwenye nguvu na uhodari
Bwana aliye hodari katika vita
Verse 4
Inueni vichwa vyenu enyi malango
Inukeni enyi malango ya kale
Mfalme wa utukufu apate kuingia
Ni nani mfalme wa utukufu?
Bwana wa majeshi
Yeye ndiye mfalme wa utukufu
Verse 5
Atukuzwe Baba na mwananna roho mtakatifu
Kama mwanzo na sasa na siku zotenna milele. Amina