SectionsExitWatikisa Kibuyu

Watikisa Kibuyu

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Nini siri ya moyo wako kupenda kuwa mtu wa roho mbaya?

Daima moyo wako wasononeka kwa kujiuliza kwa nini?

Jirani yako anapofanikiwa moyo wako wakosa raha

Si zuri si jema moyo wako wakutesa ukiwaza kwa nini!n

Chorus

Na tazama sasa- unachokifanya,

Ni kukimbilia - kutikisa kibuyu

Na imani yako - ni kwenye kibuyu na kibuyu ndiye mungu wako

Verse 3

Wengine wanakiita ni kinga na kukifanya kama mungu wao

Na tena jina jingine ni 'kimo' sababu yake na kiza ni wivu

Unajisifia ni mtu mwema mwenye roho iliyo na huruma

Lakini kwa ndani wewe mbaya roho imetawaliwa na wivu!

Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!

Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!n

Verse 4

Mtoto wa jirani kafaulu katika kazi au ni masomo

Ukijua wakiwaza kibuyu ugeuze miguu yake nyuma

Wenzako wanaongeza bidii ya kujituma kwenye kazi zao

Wewe unawatazama vibaya na kuanza kukiwaza kibuyu

Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu

Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu

Verse 5

Unapomtazama ndugu yako kajenga nyumba na inapendeza

Ukiitazama moyo wauma sasa wawaza huyu asiishi!

Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!

Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!

Verse 6

Sasa jifikirie ndugu wewe badili roho yako yenye wivu

Na kuutengeneza moyo wako ukafanane nao malaika

Ukirudi kazi kwako ni moja ni kupiga magoti na kusali

Ah! Kumbe waomba upendo uwepo duniani