Wastahili Sifa

Ordinary Time,MarianBible Procession
Chorus

{ Wastahili sifa ee Mungu huko Sioni

Watu watakutimizia wewe ahadi zao

Maana wewe wajibu sala zetu }*2

Verse 2

[s] Tunapoelemewa na makosa yetu

Wewe mwenyewe watusamehe

Verse 3

[t] Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu

Waishi katika maskani yako

Verse 4

[a] Wasababisha furaha kila wakati

Toka mashariki hata magharibi

Verse 5

[b] Wewe waitunza nchi kwa kuinyeshea mvua

Waijalia rutuba na kuistawisha