SectionsExitWangu Wa Milele

Wangu Wa Milele

WeddingExit
Chorus

Mpenzi wangu ungana nami, tumshukuru Mungu wetu

Uje tucheze kwa furaha, tumshukuru Mungu wetu

Kwani ile siku tuliyoingojea - iwe tumshukuru Mungu wetu

Mwenyezi ametujalia - iwe, tumshukuru Mungu wetu

Verse 2

Nasema mbele ya wazazi wako (ni wewe)

Ni wewe niliyekuchagua (ni wewe)

Nasema mbele ya wazazi wangu, ni we wangu wa moyoni

Ninatamka mbele za Mungu (ni wewe)

Mtima wangu nakupatia (ni wewe)

Nasema mbele ya wazazi wangu, Ni we wo mtima gwange

Verse 3

Unawaacha wazazi wako (ni wewe)

Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)

Nami nitakupenda milele, Ni we wangu wa moyoni

Ninawaacha wazazi wangu (ni wewe)

Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)

Nami nitakupenda milele, Ni we wo mtima gwangen

Verse 4

Ndi-we mama wa watoto wangu (ni wewe)

Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)

Karibu kwetu kipenzi changu, ni we wangu wa moyoni

Ndi-we baba wa watoto wangu (ni wewe)

Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)

Nakuja kwenu kipenzi changu, Ni we wo mtima gwange

Verse 5

Nawashukuru wazazi wako, umbo zuri wameniletea

Namshukuru Mwenyezi Mungu, ni we wangu wa moyoni

Nawashukuru wazazi wako, lulu yangu walinitunzia

Haki ya Mungu nitakutunza, ni we wo mtima gwange