SectionsExitWamnunia Mungu

Wamnunia Mungu

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Twajiuliza ewe ndugu yangu kwa kuyatafakari maisha yako

Mawazo hata kwa matendo yako kila siku

Upendo kwako kitu gani, amani moyoni i wapi

Si kwa maneno hata kwa matendo upendo kwako umetoweka

Verse 2

Daima wewe wa huzuni furaha imekukimbia

Huzuni kwako meshika hatamu, furaha ya moyowe i wapi

Kunapokucha ni kununa, mchana kutwa ni kununa

Giza lijapo, na mwisho wa mwezi moyo wako hauna furaha

Verse 3

Unapojiwa na mgeni, ndugu yako au rafiki hata jirani

Hakuna wa heri, karibu kwako masikitiko

Kwa mwenye jema kwako, unywe lenye baraka kwako

Shida shukrani yako, tena wanuna sasa unamnunia Mungu

Verse 4

Upatapo wanung'unika, ukosapo walalamika

Bidii ya kazi imekutoweka, lipi kwako linakuridhisha

Mwenzako anapokosea kauli kali wazipenda,

Lugha nyeusi nazo wazipenda na hiyo ndiyo furaha yakon

Verse 5

Wivu ndiye rafiki yako, dharau ndilo gari lako

Shambani mwako umepanda chuki sasa unavuna ubinafsi

Moyo wako umeulinda kwa kuuwekea uzuio

Uliojengwa kwa mawe magumu yaliyojengwa naye shetani

Verse 6

maisha gani haya ndugu yasiyokuwa na upendo

Yasiyokuwa hata na baraka kutokana na matendo yako

Jitafakari ndugu yangu mwenendo wako ubadili

Hebu jirudi kwa maisha haya au umeagana na Mungun