SectionsExitWamegawanyika

Wamegawanyika

Ordinary TimeExit
Chorus

Nikiiwaziawazia kazi yake Mwenyezi lo

Na alivyomuumba huyu mwanadamu

Tazama inavyopendeza kazi yake Mwenyezi lo

Na wengine kwa jinsi wanavyojipangan

Chorus

n{ Lakini sasa wamegawanyika

Tazama leo wao si kitu kimoja } *2

Chorus

Wengine wanatafuta upendo ili kuwajali wengine

Wengine wamefanana na yule simba mnyama mkali

Wengine watafutacho ni mali tena utu umepotea

Hakuna kiburi cha kumwaga damu ya watu wengine

Verse 4

Unapowatazama wa nje eeh eeh

Na kwa jinsi wanavyopendeza eeh eeh

Hata kwenye miondoko yao eeh eeh

Wewe mwenyewe utawapenda eeh eeh

Lakini katika nyoyo zao eeh eeh

Wako katika sura ya kazi eeh eeh

Kwa kweli katika roho zao eeh eeh

Upendo kwao ni kama chambo eeh eeh

Verse 5

Na wengine wanapojipamba eeh eeh

Utawadhania malaika eeh eeh

Nyumba magari ya kifahari eeh eeh

Mwendo wao ni wenye heshima eeh eeh

Tembea wataongea yao eeh eeh

Kwa upole upendo amani eeh eeh

Kumbe moyoni wana kikao eeh eeh

Leo iwe ni zamu ya nani eeh eeh

Verse 6

Wamezoea kupata mali eeh eeh

Bila kuwa na moyo wa utu eeh eeh

Kuwatoa wengine kafara eeh eeh

Si tatizo bora wafaulu eeh eeh

Kukata viungo vya wenzao eeh eeh

Kwao wanachojali ni mali eeh eeh

Na wengine kufanywa pepeta eeh eeh

Utu si kitu bora ni mali eeh eehn

Verse 7

Kweli wachuna ngozi wenzao eeh eeh

Sasa ni zamu ya albino eeh eeh

Tatizo la yote hayo ni mali eeh eeh

Pengine watabadili wazo eeh eeh

Na kusema sasa ni weupe eeh eeh

Kisha waseme sasa wafupi eeh eeh

Wataongeza sasa wanene eeh eeh

Wapate mali kishirikina eeh eeh