SectionsExitWakupeleka Hukumuni

Wakupeleka Hukumuni

LentExit
Chorus

Wakupeleka hukumuni Yesu,nili uamuliwe na mtu

Tendo gani umefanya Yesu,nhata wakutaka usulibiwe

Ulikuja kwangu, mi mdhambi

Ili uniokoe katika taabu zangu zote

Unipatanishe na Mungu Baba

Ili nifike kwake kwenye uzima wa milele

Chorus

Kwa nini unateseka hivyo,

Bwana usiye na kosa lolote

Mimi ndiye mwenye kosa Yesu,

Nawe ndiwe wa kunihukumu

Msalaba mzito waubeba

Mijeredi kupigwa, taji la miiba kuvalishwa

Yote umekubali, juu yangu

Ili unikomboe, mimi mdhambi wa huzunin

Chorus

n{ Nimekosa mimi nimekosa

Unihurumie Mungu wangu } *2

Verse 4

Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu

Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza

Toka mbinguni Mungu aliwachungulia wanadamu

Aone kama yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu

Verse 5

Ee Mungu kwa jina lako uniokoe

Na kwa uweza wako unifanyie hukumu,

Ee Mungu uyasikie maombi yangu

Uyasikilize maneno ya kinywa changu.n