Wakenya Tuna Furaha
Wakenya tunafuraha (tele)
Mungu kweli katubariki, nusu karne tuko imara.
Njooni tufanye shangwe,
Kwa vifijo na nderemo kuu, jubilee sherehe kubwa x2n
n(Hakika) Miaka hamsini tuna uhuru,
Tumeishi tukipendana
Kwa umoja pia amani,
Ni Baraka kuwa Mkenya x2
Makabila ya Kenya (Yote)
Yamerembesha nchi yetu, kwa nakshi za utamaduni.
Lugha zinazovutia (sana)
Zifurahishazo mioyo, na bado tunaelewana x2
Madhari yapendezayo (sana)
Milima mito na mabonde, nyufa mbuga na fuo za bahari.
Maziwa yapendezayo (pia)
Hifadhi za kihistoria, utalii tumeimarika x2
Ulinzi tuko kijeshi (ona)
Angani tuko imara, nchi maji usituchezee.
Majasusi wale wabaya (na)
Polisi tunao wa kutosha, kweli Kenya ni nchi salama x2.
Viongozi waliosoma (pia)
Sarakasi wanazielewa, walimwengu tunawatishia.
Kuwa Mkenya ni Baraka (kweli)
Tujenge nchi kwa furaha, Kenya yetu ni mimi na wewe x2