Chorus
Wakati sasa umefika, wa kutoa sadaka
Amka ndugu tupeleke, sadaka zetu kwake
Ni mema mengi sana kila siku anatugawia
Lakini tunshindwa kumshukuru Mungu Baba
Twendeni kwa pamoja tupeleke sadaka zetu
Tutoe kwa upendo Mungu Baba atapokea
Verse 2
Ee ndugu fikiria maisha yako yote
Tangu kuumbwa kwako na bado unaishi
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
Verse 3
Usiku na mchana hachoki kutulinda
Tukiwa na safari ajali aepusha
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
Verse 4
Uwezo wako wote umepewa na Mungu
Na kazi ufanyazo Mungu amebariki
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
Verse 5
Mapato yako yote yanatoka kwa Bwana
Ingawa ni kidogo Bwana atapokea
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka