Chorus
Viuzeni mlivyo navyo mtoe sadaka
Kwani mnajiwekea hazina mbinguni
Verse 2
Ziwekeni fedha zenu katika akiba ya mbinguni
Ziwekeni mali zenu katika mifuko ya mbinguni
Verse 3
Msidhani kwamba mnazipoteza mali zenu bure
Kweli kwamba mnaweka katika hazina ya mbinguni
Verse 4
Viuzeni mali zenu mtoe sadaka kwake Bwana
Viuzeni vitu vyote mweke hazina ya mbinguni
Verse 5
Rudisheni vitu vyote kwani yeye ndiye aliwapa
Aliwapa bure nanyi pia mkazirudishe bure
Verse 6
Mkatoe kwake Bwana kwa moyo mmoja na mapendo
Ni akiba mnaweka katika mifuko ya mbinguni