Basi ndugu zangu, hatimaye imetosha
Acheni kunung'unika kuhusu kifo
Jitayarisheni ili mfe kifo chema
Hiyo hekima ya kweli na ucha Mungu kamili
Kifo ni zawadi ya upendo toka kwa Mungu
Nacho kimeandaliwa kuivuka dunia chungu
Ibada na dini zenu ni upuuzi mtupu
Kama mwisho wake siyo kumfikia Mungu
Lakini hamuwezi kumfikia Mungu
Isipokuwa kwa njia hii ya kifon
Dhambi ya Adamu ilimfanya Adamu,nakajificha mbali na uso wa Mungu
Akapewa kifo,nkusudi roho yake irudi karibu na Mungu milelen
Kifo kilibeba maana yake halisi,nalipoinuliwa Mwokozi wa watu
Akashinda kifo,nkusudi watu wake baada ya kifo warudi kwa Mungu
Kama hampendi, taabu za ulimwengu,nkwa nini mwaogopa kujitayarisha
Kupokea kifo,nkusudi muiage dunia mpokee raha ya milele
Tofautisheni, kifo nayo mauti,nmauti humpeleka mwenzetu kuzimu
Ingawaje kifo,nhumtenganisha mwenzetu na taabu za dunia hii