Chorus
Uzuio wa umeme, mlinzi wa Kimasai
Mbwa mkali tunguri na silaha za kisasanhakika, hazifai kitu, kweli hazifai kitu
Bwana amtumapo mjumbe kuchukua roho yako
Verse 2
Wako wapi, wako wapi waliowahi kutikisa dunia?
Wako wapi walioita miungu na dunia?
Na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kujikinga
Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua?
Verse 3
Wako wapi, wako wapi waliowahi kuishi angani?
Wako walio ishi kwenye madaha?
Je hakuna hata mmoja wao aliyeweza kujificha
Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua