SectionsEucharistUwe Nami Bwana

Uwe Nami Bwana

Ordinary Time,MarianEucharist
Verse 1

Ninakushukuru ee Mungu Babanna kukusifu ewe mfalme wangu

Kwa sauti kuu tamu na za furahannacheza kwa madaha mbele yako Bwana

Nakushukuru kwa mema yote uliyonitendea mimi maishani mwangu.

Chorus

Nakukaribisha (mimi) uwe nami Bwana (Yesu)

Uishi na mimi, Bwana daima milele.

Wewe Mungu mwema (kweli) na mwenye fadhili (nyingi)

Umenikubali japo mimi mwenye dhambi.n(Nakushukuru kwa kuniita kwako

Niwe mmoja wako daima milele x2)

Verse 3

Umenipa mwili wako ee Bwananchakula chenye uzima wa milele

Kikombe cha damu yako nimekunywankinywaji safi kinachonitakasa

Sitaona njaa wala kiu mimi maana u ndani ya roho yangu

Verse 4

Nafsi yangu yakutafuta Bwanankama ayala aonavyo kiu ya maji

Usiende mbali na mimi Bwananmaana ndiwe ngao ya maisha yangu

Na nguzo ya uhai wangu, tena wewe Bwana ndiwe tegemeo langu

Verse 5

Ee Bwana unaijua nafsi yangunna siri zote zilizo moyoni mwangu

Umezitakasa doa zangu zotenmimi ni kiumbe kipya mbele yako

Najitoa mimi kwako Bwana unitumie jinsi utakavyo wewe