Verse 1
Utukufu kwa Mungu juu
Na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema
Chorus
Mungu tunakusifu
Mungu tunakuheshimu
Mungu tunakuabudu, tunakutukuza
Verse 3
Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu
Ee Bwana Mungu, mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba mwenyezi
Verse 4
Ee Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee,
Ee Bwana Mungu,nmwana kondoo wa Mungu mwana wa Baba
Verse 5
Mwenye kuondoa dhambi za dunia, utuhurumie
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia,npokea ombi letun
Verse 6
Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie,
Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako mtakatifu
Peke yako Bwana peke yako mkuu Yesu Kristun
Verse 7
Pamoja na roho mtakatifu
Katika utukufu wa Mungu Baba amina.n