Verse 1
Utukufu kwa Mungu Baba juu mbingunin
Chorus
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni na amani
Amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema
Verse 3
Nayo sifa na heshima tunakupa wewe
Na ibada, utukufu pia kwako wewe
Verse 4
Ewe Bwana ndiwe mfalme juu mbinguni
Bwana Mungu Baba, Baba mwenyezi
Verse 5
Ewe Bwana ndiwe mfalme juu mbinguni
Bwana Mungu mwana kondoo wa Mungu Bwana
Verse 6
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
Twakuomba ee Bwana utuhurumie
Verse 7
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
Twakuomba upokee ombi letu Bwana
Verse 8
Ewe mwenye kuketi kule kuume
Kuume kwa Mungu Baba utuhurumien
Verse 9
Peke yako mtakatifu, peke yako Bwana
Peke yako u mkuu Yesu Kristu
Verse 10
Pamoja naye Roho, Roho Mtakatifu
Katika utukufu wake Mungu Baba