SectionsEucharistUtukufu Kwa Mungu (Iii)

Utukufu Kwa Mungu (Iii)

Ordinary Time,MarianEucharist
Verse 1

Utukufu kwa Mungu, na amani duniani

Kwa watu wenye mapenzi mema

Kwa wenye mapenzi mema

Verse 2

Tunakusifu Bwana tunakuheshimu

Twakuabudu Bwana tunakutukuza

Twakushukuru Baba Mwenyezi mfalme wa Mbinguni

Verse 3

Ewe Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee

Mwanakondoo wa Mungu, mwana wake Baba

Uondoaye makosa yetu tuhurumie

Verse 4

Tunakusifu Bwana utusikilize

Wewe unayeketi kuume kwa Baba

Ni pekee Bwana ni mtakatifu mkuu Yesu Kristun

Verse 5

Pamoja naye Mungu, Roho Mtakatifu

Katika utukufu wake Mungu Baba

Milele yote milele yote amina amina