Verse 1
Utukufu kwa Mungu juu mbingunin
Chorus
Tunakusifu tunakuheshimu
Tunakuabudu tunakutukuza.
Verse 3
Tunakushukuru Mungu kwa ajili
Ya utukufu wako mkuu, Ee Bwana ni Mungu
Ndiwe mfalme wa mbinguni.
Verse 4
Ee Baba mwenyezi Bwana Yesu Kristu
Ee mwana wa pekee ee Mungu Mwanakondoo
Wa Mungu mwana wake Baba
Verse 5
Mwenye kuondoa dhambi za dunia
Utuhurumie, tuhurumie maombi yetu
Bwana uyapokeen
Verse 6
Mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie
Kwa kuwa ndiwe peke yako ni Mtakatifu
Verse 7
Peke yako Bwana peke yako mkuu
Ewe Yesu Kristu, Pamoja naye Roho Mtakatifu
Milele yote.