SectionsEucharistUtukufu Juu Kwa Mungu (Misa Kariobangi)

Utukufu Juu Kwa Mungu (Misa Kariobangi)

Ordinary Time,MarianEucharist
Chorus

Utukufu juu kwa Mungu, Utukufu juu Mbinguni

Na amani kote duniani, Kwa wenye mapenzi mema

Verse 2

Tunakusifu tunakuheshimu, tunakuabu tunakutukuza

Twakushukuru kwa ajili, ya utukufu wako mkuu

Verse 3

Ewe Mungu ndiye mfalme, wa mbinguni Baba mwenyezi

Ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee mwana wa baba

Verse 4

Ewe Yesu mwanakondoo, wa Mungu mwana wa Baba

Ewe mwenye kuziondoa, dhambi zetu tuhurumie

Verse 5

Ewe mwenye kuziondoa, za dunia dhambi za watu

Ewe mwenye rehema nyingi, upokee maombi yetun

Verse 6

Uketiye kuume kwake, Mungu Baba tuhurumie

Kwa kuwa ndiwe uliye, peke yako Mtakatifu

Verse 7

Peke yako ni wewe Bwana, peke yako Bwana mkuu

Peke yako ni mkombozi, peke yako Yesu Kristun

Verse 8

Naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake

Mungu mmoja anayeishi, na kutawala milele yote.n