SectionsExitUtanisahau Kabisa Mpaka Lini

Utanisahau Kabisa Mpaka Lini

LentExit
Verse 1

Ee Mwenyezi Mungu utanisahau kabisa mpaka lini?

Utauficha uso wako mbali nami mpaka lini Mungu wangu?

Verse 2

Roho na mwili wangu vitakuwa na wasiwasi mpaka lini?

Na masikitiko siku hata siku sina raha maishani

Verse 3

Bwana nimelia sana, mchana uko wapi unifadhili

Na usiku usingizi sipati nakesha nikiwaza

Verse 4

Nimedhoofika sana fimbo kila siku nachapwa nimekonda

Sina pa kukimbilia njia zote zimelindwa niende wapin

Verse 5

Maadui zangu ni wengi, njaa magonjwa ya hatari na ajali

Vita vimepamba moto dunia yote ona Bwana ninavyotishwa

Verse 6

Ndugu na rafiki zangu wametoweka siwaoni wako wapi

Kama wako kwako Bwana nambie nami nijaribu kuwafuata

Verse 7

Yesu wangu u Mungu wangu njoo haraka nakuita njoo Bwana

Mwanao nateseka sijiwezi mimi ninaomba msaada wako

Verse 8

Ninainua mikono taabu mateso maumivu yangu yote

Ninakukabidhi wana yapokee Mwokozi naomba usinitype