SectionsThanksgivingUshuhuda Tosha

Ushuhuda Tosha

Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Tuna haki ya kutamka na kutoa ushuhuda

Mambo mema alotenda Mungu pia na kwa huruma

Ninamwambia naye jirani Mungu ana huruma

Chorus

{ Ushuhuda, huo ni ushuhuda tosha (nasema)

Ni huruma, Mungu ana huruma nyingi (hakika)

Ninapolala pia ninaamka huo wote ni ushuhuda tosha } *2

Verse 3

Kaumba mbingu na dunia wanyama hata samaki

Binadamu na akili nyingi sisi tukawatawale

Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu

Verse 4

Tunalala bila kuomba hatimaye twaamka

Mungu wetu na hakasiriki bado atupa mkate

Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu

Verse 5

Maisha yetu twayapanga nayo yanafanikiwa

Mara nyingi hata hatuombi kumshirikisha Mungu

Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu

Verse 6

Tunapofanya biashara uongo tunatumia

Twazikiuka amri za Mungu ili tupate faida

Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu

Verse 7

Ni mengi hatujatamka wanadamu tunafanya

Tunaomba msamaha Mungu sisi sote walegevu

Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu