SectionsExitUpendo Na Ukarimu

Upendo Na Ukarimu

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Watu wengi tunajaribu upendo

Tunawajali wale wanaotuhusu

Tunaojua wataweza kutulipa

Hatuwathamini wale wasiotuhusu

Wala wasiojiweza, lakini

Chorus

{Leo tumejifunza wote,nupendo ni kitu gani (wapendwa)

Tena tumepewa mfano,nukarimu una sifa gani (wapenzi) } * 2n

Verse 3

Tunawakopesha wenye kipato kikubwa

Tukiamini nao watatukopesha

Wakitujia wenye shida na fukara

Tunawakimbia eti hawakopesheki

Na wana madeni mengi, lakini

Verse 4

Wakiugua wenye nafasi za juu

Tunajazana kwao na vichupachupa

Tukiamini na sisi tukiugua

Watalundikana kwetu na vifuko fuko

Kadi na michango mingi, lakini

Verse 5

Tukitembelewa na mtu mwenye viraka

Tunauliza kama tulimualika

Akija aliyeshuka kwenye shangingi

Tunamwuliza kinywaji anachokunywa

Tena kwa unyenyekevu lakini