SectionsThanksgivingUpendo Kupita Upeo

Upendo Kupita Upeo

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Ee Mungu wangu, kwa hakika unanipenda

Upeo wa macho yangu, sijui nikulipe nini

Maisha yangu, nayatazama nashukuru

Kwa yote uliyotenda, na pale uliponitoa

Chorus

Ningelikuwa natazama ya binadamun(hakika leo) fadhila yake ingelikuwa madharau

Lakini wewe utoaye hewa na majin(watugawia) tajiri hata walemavu na maskini

Verse 3

Na marafiki, walinipenda wengi sana

Nilipokuwa na gari na nyumba yenye kupendeza

Walinipenda, pale pesa zilipoisha

Majuto niliyapata, nilipoachwa peke yangu

Verse 4

Maisha yangu, yalipokuwa yenye shida

Hakika ulinitoa, nilipoanguka shimoni

Baraka nyingi, ulimimina kwangu mimi

Hata nao majirani, sasa wamebaki butwaa

Verse 5

Ninashukuru, kwa kunikinga na ajali

Ninaposafiri mimi, umekuwa dereva wangu

Pia magonjwa, umeyapiga teke kwangu

Hakika nina sababu, ya kutamka sifa zako