Chorus
{ Ewe mwenzangu univishe pete kwenye chanda changu,
Iwe ni alama ya uaminifu wako } *2
Verse 2
Naapa mbele ya Mungu, mimi ni wako siku zote,
Nitamuacha Baba nitamwacha na mama
Niambatane nawe, nasi tutakuwa mwili mmoja
Verse 3
Wewe sio malaika ni mwanadamu kama mimi,
Makosa kawaida tuko sawa maumbile
Maumbile ya Mungu, nitakusamehe ukinikosea
Verse 4
Macho yangu yameona, yameona wengi sana,
Kati yao wengi, ninakuvika pete
Iwe alama yangu ya uaminifu wangu kwako