SectionsExitUniokoe Uniokoe

Uniokoe Uniokoe

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Unioke uniokoe na watu hao wabaya

Na unikinge unikinge na wakatili

Wenye mawazo mabaya *2

Verse 2

Daima hao huzusha ugomvi

Na ndimi zao hatari kama nyoka

Midomo yao maneno hatari

Ni kama sumu hatari ya joka

Mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwa kucha zao wabaya na katili

Verse 3

Wenye kiburi hutega

Mipango yao waone uanguke

Wametandaza kamba kama wavu

Njiani wamezificha mitego

Mipango yao yote wanikamate

Sauti ya ombi langu sikiliza

Verse 4

Mkombozi mkuu wangu umenikinga

Salama hata wakati wa vita

Waovu usiwape wanayotataka

Mipango yao mibaya huivunje

Wameinua kucha wamenizingira

Uovu wao wenyewe uwapate