Verse 1
Hufanani nasi, unang'ara na tena una enzi, una utukufu
Umepita zote, sifa tunazokutolea sisi, nao malaika oho
Chorus
Wewe uko juu umetukuka na tunakuinua kwa nyimbo zetu hizi
Verse 3
Walikuimbia, baba zetu lakini hazikwisha, sifa zako wewe
Na watakatifu, wanaimba na hazimaliziki, tenzi hazitoshi oho
Verse 4
Mimea ya nchi, yaeleza inapopukutika, kuhifadhi maji
Kwamba wewe Bwana, hupungui unajua kuumba, hupitiwi neno oho
Verse 5
Kinyonga mdogo, anageuka rangi kujilinda, bila ya bunduki.
Anafafanua, umakini ndani ya kazi yako, isiyo dosari ohon
Verse 6
Na uhimidiwe, wewe Baba yaani ndiwe Mwana, Roho Mtukufu,
Ulivyotukuzwa, enzi zile sasa hata milele, utukuzwe pote ohon