SectionsExitUkiaona Kama Watu

Ukiaona Kama Watu

Ordinary TimeExit
Chorus

Ukiwaona kama watu - hao, kama watu

Kumbe ndani ni mbwa mwitu - hao, mbwa mwitu

Wamejivika mavazi ya kondoo * 4

Verse 2

Sura zao zinavutia machoni pa watu

Na kuonekana wao ni wa maana kwa watu

Matapeli wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu

Wala rushwa wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu

Verse 3

Vinywa vyao hunena maneno matamu kwa watu

Na kuonekana wenye hekima nyingi kwa watu

Kumbe ndani hao ni wachafu (wachafu *2) wanadamu

Wanadhani Mungu hawaoni (wachafu *3) wanadamu

Verse 4

Kwa ushirikina wao ni viongozi hodari

Hujisifia kwa mambo yao maovu kwa watu

Kumbe wanajilisha upepo mchafu

Kwa hivyo unayo hii (nafasi *2) kwa Mungu mwanadamu

Verse 5

Ufisadi uso na mfano ni wao ni wao

Ukiwaona wala huwezi dhania ni wao

Kweli ndugu inasikitisha, ni wao, ni wao wanadamu

Hawamuogopi hata Mungu ni wao ni wao wanadamu

Verse 6

Nyumba za ibada hawakosekani, kwa kweli

Na nyadhifa pia wanajitwalia aibu

Mnamdhalilisha Mungu, Mungu, Mungu, wanadamu

Elewa Mungu anakuona, kuona, kuona, mwanadamu