SectionsEntranceUje Roho Mtakatifu Tuangaze

Uje Roho Mtakatifu Tuangaze

PentecostalEntrance
Verse 1

Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu

Roho zetu kwa mwangao

Verse 2

Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji

Uje mwanga wa mioyo

Verse 3

Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana

Ewe raha mustarehen

Verse 4

Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudiko

U mfutaji wa machozi

Verse 5

Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini

Neema yako mioyoni

Verse 6

Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu

Kwake yote yana kosa

Verse 7

Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu

Na kuponya majerahan

Verse 8

Ulegeze ukaidi, washa moto wa uadili

Nyoosha upotevu wote

Verse 9

Wape waumini wako, wenye tumaini kwako

Paji zako zote saba

Verse 10

Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila

Wape heri ya milele

Verse 11

Amina aleluya, amina aleluya,

Amina aleluya