Chorus
Ujana ni maji ya moto bila Mungu ni majuto
Ujana ni maji ya moto ukicheza utakuchoma
Kunapokucha ni raga
Mwili bado una nguvu nyingi
Tunapomsahau Mungu vijana twapotea *2
Verse 2
Vishawishi ni vingi mno, ili tupate pesa nyingi
Wengine tunaua ili tupate pesa
Twaharibu amani ili tupate pesa
Tunapomsahau Mungu vijana twapotea
Verse 3
Magaidi wanatutumia, twauana sisi kwa sisi
Jamii inalia machozi ya uchungu
Wasio na hatia wauawa kwa nini
Tunapomsahau Mungu vijana twapotea
Verse 4
Ndoto zetu zinakatizwa, na wale wasio na utu
Wasiwasi kazini, wasiwasi shuleni
Mjini wasiwasi twatembea kwa hofu
Tunapomsahau Mungu vijana twapotea