SectionsExitUhuru Wa Kweli

Uhuru Wa Kweli

Ordinary TimeExit
Verse 1

//utangulizin

Ninyi mliitwa ndugu muwe watu huru kabisa

Lakini uhuru huo sio wa kuusingizia

Isiwe ni sababu - ya kutawaliwa na tamaa hizi

Tamaa za dunia - msitawaliwe na tamaa za dunia

Ooh jifunzeni kutumikiana kwa upendo daima

Kwani sheria ni moja nayo ndiyo upendo

Chorus

n//kiitikio

Uhuru wangu ee - uhuru wangu

Uhuru wangu wa thamani

Uhuru wangu jamani - uhuru wangu (uhuru)

Unatokana na ukweli

Verse 3

Nikijisifu kwa uongo, nateseka

Kwani siwezi dhihirisha sifa yenyewe

Jamii itatarajia kutoka kwangu

Nisiyoweza kuyatenda, kwani si ya kweli!

Verse 4

Nikifanya udanganyifu, kwenye fedha

Nikimwona ausikaye ninazizima

Au nikipokea rushwa, nitanena

Hata yale yasiyo mema, yanidhalilishe!

Verse 5

Nikikosa uaminifu, kwenye ndoa

Nitakwepa kuongozana, na mpendwa wangu

Ili tusije kukutana, na hawara

Akashindwa kuvumilia, akanipondeza!

Verse 6

Nikizunguka nchi nzima, kuongea

Uwogo juu ya mwenzangu, najiumiza

Tukikutana ana njaa, yuko kimya

Nitadhani wamemwambia, nitapata hofu

Verse 7

Nikimtesa mpwa wangu, nimleaye

Sitatamani aonane na wazazi wake

Kwani najua atasema, nimtendeayo

Na mimi nitadhalilika, nitaaibika!

Verse 8

Nikifanya upendeleo, ofisini

Kumkweza asiyefaa, najidhihaki

Jamii ikimhubiri, afaaye

Nitahisi nakejeliwa na kuunguliwan

Verse 9

n// hitimishon---

Kwa sababu mimi, ndiye, ninaiandika mwenyewe

Historia yangu, leo, itakayosomwa milele

Daima milele, daima milele, daima milele

Muamuzi wangu ndimi!