Chorus
Ufurahi moyo wao, wamtafutao Bwana *2n{ Mtafuteni Bwana, na nguvu zake
Utafuteni uso wake siku zote } *2
Verse 2
Kwa nyimbo nzuri na ngoma tamu, kwa vinubi pia vinanda,
Tupige makofi tumtukuze Mungu mwenye uwezo
Mshangilieni, mwimbieni Bwana
Usimulieni ukuu wake siku kwa siku
Verse 3
Simameni wababa wote, inukeni na kina mama
Vijana wacheze na watoto warukeruke leo
Msifuni Mungu, mwabuduni Yeye,
Tafuteni Bwana maana anapatikana
Verse 4
Lisifieni jina takatifu, nyanyukeni viumbe vyote
Zikumbukeni ajabu na hukumu ya kinywa chake
Msifuni Mungu, mwabuduni yeye
Mwambieni Yahweh, matendo yake yanatisha
Verse 5
Mshukuruni Mwenyezi Mungu, tangazeni ukuu wake
Yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda
Mshangilieni, mwambieni Bwana
Msimulieni matendo yake ya ajabu.