Verse 1
{ Twendeni tuingie kwake
Na nyimbo nzuri za shangwe } *2
Verse 2
Dunia nzima imshangilie Bwana
Kwa furaha tumtumikie wote
Tumwendee na nyimbo za shangwe
Verse 3
Mjue Bwana wetu ni Mungu
Ametufanya na tuko watu wake
Sisi kondoo wa malisho yake
Verse 4
Ingieni mlangoni kwa kumsifu
Nyumbani mwake tumtolee heshima
Tutukuze jina lake kubwa mno
Verse 5
Kweli Mungu kwa Baba mwenyezi
Na kwa mwana Mwokozi wetu
Na kwa Roho Mtakatifu ndani mwetu