Twausifu Moyo Wako Maria
Twausifu, moyo wako Mama Maria, (moyo mwema )
Twauheshimu, moyo wako mama Maria (moyo safi)
Moyo wako Maria usio na doa
Moyo wako Maria usio na doa
Moyo wako Mama una faraja
Unang'ara sana unavyopendeza
Moyo wako Mama mpenzi Maria
Ni msafi kweli unameremeta
Moyo wako mama, umekingiwa
Dhambi ya asili tuliyoirithi
Moyo wako mama ni mtakatifu
Umejaa neema neema teletele
Moyo wako mama, kama waridi
Unafurahisha unametameta
Moyo wako mama, kama dhahabu
Ing'arayo sana mfano wa kioo
Moyo wako mama, ni mtii sana
Moyo wako mama mtulivu kabisa
Moyo wako mama ni nuru njema
Ituongozayo kufika Mbinguni
Moyo wako mama, ni mnyenyekevu
Moyo wako mama una heri tele
Moyo wako mama ni wa amani
Moyo wako mama una neema ya Mungu
Tuombee mama yetu Maria
Tuombee mama kwa mwanao Yesu
Ili atakase mioyo yetu
Ifanane nawe mama yetu mpenzin