SectionsExitTwakukimbilia Maria

Twakukimbilia Maria

Marian,Marian,Marian,Marian,Marian,MarianExit
Verse 1

Twakukimbilia Maria,

Mama Bikira mwenye huruman tutie nguvu ya safari tufike

Chorus

Kwa mwanao Yesu Kristu

Angaza njia mama Maria

Tufke makao ya uzima

Giza limeyafunika macho mama Maria

Mama Maria twapotea

Tunahitaji msaada wako mama Maria

Mama Maria tuone njia

Verse 3

Safari ni ngumu Maria

Shetani mwovu atusumbua

Hatua ni nzito Maria

Miguu yetu imelegea

Verse 4

Utupe nguvu Maria

Ili tusije vunjika moyo

Tuwe shupavu na imara

Katika safari hii ya roho

Verse 5

Utuombee kwa mwanao

Tupate nguvu kumshinda shetani

Tujikane tujute dhambi

Tuweze kufka kwake mbinguni