SectionsExitTwakukimbilia Maria Mama

Twakukimbilia Maria Mama

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Pentecostal,Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Twakukimbilia Maria, mama Bikira mwenye huruma

Tutie nguvu ya safari, tufike kwa mwanao Yesu Kristu

Chorus

Angaza njia Mama Maria,

Tufike makao ya uzima

Giza limeyafunika macho

Mama Maria Mama Maria, twapotea,

Tunahitaji msaada wako

Mama Maria Mama Maria, tuone njia

Verse 3

Safari ngumu Maria, shetani mwovu atusumbua

Hatua ni nzito Maria, miguu yetu imelegea

Verse 4

Utupe nguvu Maria, ili tusije vunjika moyo

Tuwe shupavu na imara, katika safari hii ya roho

Verse 5

Utuombee kwa mwanao, tupate nguvu kumshinda shetani

Tujikane tujute dhambi, tuweze kufika kwake mbinguni